Na Anwar Binde
Timu inayoshika nafasi ya nne leo itasafiri hadi nyumbani kwa Everton pale wanapokwenda kujaribu kurudi katika hali ya ushindi hasa baada ya kupoteza mchezo wao wiki iliyopita dhidi ya chelsea.
Everton waliokatika kiwango kizuri baada ya kushinda michezo mnne na kutoka sare mmchezo mmoja katika michezo yao mitano iliyopita wanakuta na united ambayo pia inarekodi nzuri yah iv karihun baada ya kushinda michezo mitano na kupoteza mmoja katika michezo sita waliocheza,pia wanataka kuendelea kumfukuzia arsenal katika zile nafasi za juu ili waweze kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya.
Everton waliipiga man Utd nje ndani msimu uliopita lakini msimu hh wapo vizuri chini ya uongozi wa Louis va Gaal na mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 2-1 pale jijini Manchester .Everton inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza.
Timu ya Everton itamkosa kiungo mshambuliaji Steven pienaar anasumbuliwa na misuli na viungo wengine Leon Osman aliekua ansumbuliwa na nyonga na James Mc carthy aliyekua anasumbuliwa na enka wote walirudi mazoezini.pia mshambuliaji Lomeo lukaku bado anawalakini wa kucheza mchezo huo.
Manchester United bado ina idadi kubwa ya majeruhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya safari hiyo ya Goodison, Phil Jones bado anasumbuliwa na enka, Marcos Rojo , Rafael na kiungo Michael Carrick wote hawatapatikana kwa ajili ya mchezo huo.
Jonny Evans anarudi kutoka kusimamishwa kwa kadi nyekundu, lakini kuna mashaka juu ya kiungo Daley Blind na maumivu ya enka na Adnan Januzaj pia nae enka.
Comments
Post a Comment