Na Anwar Binde,
Arsene Wenger atajaribu kumaliza uteja wake kwa Jose Mourinho pale Arsenal watakapowakaribisha chelsea katika uwanja wa Emirates pale jijini London.
The Gunners ambao mwaka 2015 ndio timu pekee katika ligi ya uingereza kukusanya pointi nyingi zaidi ya timu nyingine yoyote.wanajikuta wakiwa ponti 10 chini ya vinara wa ligi hiyo chelsea na kijaribu leo kupunguza pengo hilo ili kubakia na matumaini ya kunyakua kombe hilo,
Japokua Arsenal walipoteza mchezo wao uliopigwa mwezi oktoba mwaka jana kwa kufungwa 2-0 na Arsenal wameshinda mechi mbili katika kika mechi 12 walizokutana,na Arsene Wenger hajawahi kumfunga Jose Mourinho pale anapokua mpinzani wake katika mechi yoyote.
Mourinho ana matumaini ya kuendeleza ubabe wake kwa majirani zake hao wa jiji la London na kuondoka na pointi zote tatu na kijiongezea wigo mpana wa kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya uingereza msimu huu wa 2014/2015.
Katika mchezo huo pia tunatarajia kumuona kapteni wa zamani wa Arsenal akirudi Emirates kwa mara ya kwanza lakini akiwa na timu pinzani na pia tutaona akijaribu kuongeza rekodi yake ya kuassist na kufikia 16.
Per Mertesacker anamashaka ya kucheza kwa sababu ya kuumia kifundo cha mguu wakati wa mehi ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Reading.
Gabriel Paulista yupo fit kuanza mchezo huo. Kipa David Ospina, Hector Bellerin na Nacho Monreal, wanatarajiwa kurudi,na walikua wamekaa benchi wakati wa mechi ya nusu fainali pale wembley.
Kapteni Mikel Arteta anasumbuliwa na enka na kiungo Alex Oxlade-Chamberlain bado anamaumivu ya nyonga na hayupo vizuri,
Mourinho atafanya uamuzi wa mwisho juu ya kama mshambuliaji wake hatari Diego Costa ambae bado ni hajapona kabisa kucheza pale Emirates.
Costa amekosa mechi mbili za mwisho, lakini inaweza kurudi na kuchukua nafasi ya Didier Drogba, ambaye yupo fit baada ya kuumia enka,
Mshambuliaji Loic Remy atakua nje kabisa , hivyo Dominic Solanke inaweza kuwa benchi skama Costa atashindwa kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment