Tutamfunga Chelsea nyumbani


Tutamfunga Chelsea nyumbani

arsenal 11

Arsenal itawakaribisha majirani zao wa jijini London klabu ya Chelsea katika mchezo wa ligi utakaopigwa jumapili pale Emirates nyumbani kwa Arsenal.

Mchezo huo utakua ukimrudisha mchezaji kipenzi cha mashabiki Cesc Fabregas kwa mara ya kwanza tangu aliporudi katika ligi kuu nchini uingereza na pia kwa mara ya kwanza katika uwanja huo wa Emirates.

arsenal 4

Kocha mkuu wa Arsenal amejinadi kwmba japokuwa wana rekodi mbovu kabisa dhidi ya mahasimu wao hao wa jijini London tangu bosi wao mpya Jos Mourinho alipoichukua mikoba hiyo kwa kucheza nae michezo kumi na mbili lakini wao kuambulia patupu zaidi ya sare.Katika michezo 12 Arsenal wamepata sare 5 na kupoteza  mchezo 7.

Arsenal Wenger amedai rekodi hiyo mbovu haina madhala yoyote katika kuelekea mchezo wa jumapili na kujinasibu kwamba ataondoka na pointi zote pale nyumbani

arsenal 2

Klabu hiyo yenye maskani ya jijin londoni itaingia kwenye mchezo huo  huku ikikosa huduma ya wacezaji wake wawili  Alex-Chamberlain na Mikel Arteta wote ni majeruhi pia beki wake Per Mertsacker kuwa mguu ndani mguu nje kucheza mechi hiyo.

Timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 10 na vinara Chelsea wataingia uwanjani wakiwa na morali kubwa sana hasa kutokana na uwezo mzuri wa Arsenal ulioonyesha hivi karibuni kwa kushinda mechi nane mfulilizo

 



Comments