Tupambane mpaka dakika ya mwisho tuone nini kitatokea-kocha Prisons


Tupambane mpaka dakika ya mwisho tuone nini kitatokea-kocha Prisons

makata-march6-2015

MBWANA Makata, kocha mwenye uzoefu wa kufundisha timu za majeshi safari hii amepewa jukumu la kuibakisha Tanzania Prisons ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

Makata, kocha wa zamani wa JKT Ruvu na JKT Oljoro jana ameiongoza Prisons kupata sare nyumbani ya goli 1-1 dhidi ya Wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Baada ya sare hiyo, Makata amesema: "Mechi ilikuwa ni muhimu kwetu kuweza kupata matokeo ya ushindi, lakini mechi ilikuwa ngumu na tumeweza kutapa sare ya goli 1-1. Kikubwa niwapongeze vijana wangu kwasababu ratiba kwetu ilibana wiki hii, tulicheza jumatano, tukawa safarini na kucheza tena leo (jana), muda wa maandalizi haukuwepo. Cha msingi niwaombe wakazi wa Mbeya, mashabiki wa Prisons waisapoti timu yao, tupambane mpaka dakika za mwisho tuone nini kitatokea"



Comments