MLINZI wa kushoto wa Mtibwa Sugar, David Charles Luhende amesema mechi tatu zilizobaki ambazo zote wanacheza nyumbani watafanya vizuri na kushika nafasi za nne za juu katika msimamo.
Luhende alisema hayo jana baada ya timu yake kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya.
"Pointi moja sisi tunaona inatutosha kwasababu madhamuni yetu ilikuwa ni kushinda , lakini mwamuzi mwenyewe alivyochezesha mechi kila mtu ameona, sasa tumefikisha pointi 29, tunarudi nyumbani kucheza mechi zetu tatu zilizobaki na mungu atasaidia kubaki kwenye ligi", Amesema Luhende na kusisitiza: "Mwanzoni tulikuwa tunapambana ili tuchukue ubingwa, ligi ilisimama na tukaa nyumbani kwa muda mrefu na tuliporudi tena kambini Mungu hakutupa bahati, kila tulipokuwa tunacheza mchezo tulikuwa tunapoteza kwa bahati mbaya, Mungu katujalia leo tumepata pointi moja na mechi zilizobaki tutashinda, tuna uhakika wa kubaki ligi kuu na kuchukua nafasi nne za juu".
Comments
Post a Comment