Tottenham Hotspur inajipanga kufanya uhamisho wa beki kinara wa mabao kutoka klabu ya Torino ya Italia, Kamil Glik na imetuma wasaka vipaji wake kumtazama akifanya mambo yake dimbani.
Spurs imedhamiria kuimarisha safu yake ya ulinzi wakati Younes Kaboul akijiandaa kuondoka kiangazi hiki na inaamini sentahafu huyo raia wa Poland ni chaguo sahihi.
Glik mwenye umri wa miaka 27 ndiye kinara wa mabao miongoni mwa mabeki wanaocheza katika ligi kubwa za Ulaya akiwa na mabao nane katika mechi 33 alizocheza hadi sasa msimu huu.
Wolfsburg ya Ujerumani pia inamtaka beki huyo, lakini kwa mujibu wa mtandao wa Talksport, Spurs inajiamini kufanikisha dili lake.
Comments
Post a Comment