Klabu ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015 vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo.
Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.
Comments
Post a Comment