Real vs Atletico preview: Benzema, Bale na Modric wote nje.


Real vs Atletico preview: Benzema, Bale na Modric wote nje.

champions-league-badge-preview-real-madrid-juventus_3293013

Real madridi wana kazi ya ziada kuwazuia wapinzani wao wa jadi katika mchezo warobo fainali ili waweze kufuzu na kuendelea raundi inayofuata ya robo fainali kwa mara ya tano mfululizo.

Golikipa  Jan Oblak alikuwa shujaa wa  Atletico katika mechi ya kwanza katika uwanja wa Vicente Calderon kwa kunyima ushindi mabingwa wa Ulaya Real  katika mchezo ulipigwa pale nyumbani kwa Atletico  Vicente Calderon na  kumalizika 0-0.

 

Kijna huyo wa kislovenia mwenye umri wa miaka 22 alimyima mshambuliaji ghali zaidi duniani Gareth Bale nafasi mbili za wazi ambazo angefanikiwa kuzitumia vizuri basi kazi ingekua rahisi sana pale Santiago Bernebeu

 

Los Rojiblancos  wamepigwa mara nne na  majirani zao na kutoka sare mara tatu hii ni katika kulipiza kisasi  kwa sababu fainali ya mabigwa msimu uliopita, ambapo Real alishinda 4-1 baada ya muda wa ziada. Real, ambao wamekuwa wakiandamwa na  majeruhi  pamoja na kusimamishwa kwa wachezaji muhimu, watakuwa wanakabiliana na safu bora ya  ulinzi  Ulaya pale Santiago Bernabeu .

Atletico wameruhusu goli moja tu katika michezo yao nane  ya ligi ya mabingwa na kushinda michezo mnne kati ya sba waliyukuta na majiranizao hao. 

Real kiungo James Rodriguez anatarajia mchezo sana wa raundi ya pili ya  mapambano dhidi ya wapinzani wao Jumatano usiku. "Tunatakiwa  kuonyesha kiwango cha juu kabisa na umakini mkubwa, kucheza vizuri, (sisi lazima ) wote kitu kimoja. Nadhani kwamba kama sisi tutafanya hivyo basi tutaweza kupata  matokeo bora , "Rodriguez aliiambia tovuti ya klabu Rodriguez aliongeza: . . . " Atletico ni timu kali sana ambayo ni bora katika sehemu ya nyuma na ni kitengo muhimu katika timu,daima hapa kuna shinikizo la kujua jinsi ya kushughulikia hilo, Sisi tunakwenda kutoa kila tuliwezalo ili kuhakikisha kuwa tunashinda"  Wakati huohuo mshambuliaji wa Atletico  Antoine Griezmann , anamini kwa upande wake kuonyesha upinzani na  nguvu dhidi ya Real na ushindi ni jambo la muhimu kabisa.

karim-benzema-football-real-madrid-la-liga_3264677

Real Madridi watakosa huduma ya mshambuliaji wake karim benzema na luka Mordic ambao wote wameumia pia Marcelo amesimamishwa kitokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Atletico watakua na huduma ya mshambuliaji wao anaetajw kama ni mrithi wa Diego Costs kwa upambanaji wake Mario Mandzukic ambaye anatarajiwa kusimama na Antoine Griezmann pale mbele.

 



Comments