Real Madrid na Atlético de Madrid zinasubiriwa na kitanzi cha kufungiwa kufanya shughuli zote za uhamisho wa wachezaji katika kipindi cha misimu miwili ya usajili ijayo.
Kwa mujibu wa vituo viwili vya redio vya Hispania - Cadena SER na Cadena COPE, timu hizo zitafungiwa kusajili kuanzia dirisha lijalo la majira ya kiangazi na lile la majira ya baridi.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeamua kuchukua uamuzi sawa na ule lililoutoa kwa klabu nyingine ya Hispania, Barcelona.
Baada ya mjadala mkubwa FIFA imefikia hitimisho kwamba klabu zote mbili kutoka Jiji la Madrid zina hatia ya kuendelea kuvunja sheria inayosimamia usajili wa wachezaji wenye umri mdogo.
Comments
Post a Comment