RAIS WA BARCELONA AINGIA MZIGONI KUHAKIKISHA DANI ALVES HAONDOKI



RAIS WA BARCELONA AINGIA MZIGONI KUHAKIKISHA DANI ALVES HAONDOKI

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu ameamua kulivalia njuga suala la Dani Alves kwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na wakala wake katika harakati za kujaribu kumbakisha beki huyo katika klabu yake.
Bartomeu amechukua uamuzi wa kukutana na wakala huyo, Dinorah Santana, baada ya mwanamama huyo kufichua kwa vyombo vya habari ofa ya klabu hiyo na kuitangazia dunia kwamba mteja wake ataondoka.
Bartomeu anajua kwamba Alves anataka kubaki na yuko tayari kushikiza hilo kwa hata kuweka mezani kiasi cha fedha ambacho PSG imemtangazi beki huyo ili ajiunge nao.
Klabu hiyo ya Ufaransa imekubali dili la miaka mitatu kwa Mbarazil huyo lenye thamani ya euro milioni 9 kwa msimu kabla ya kodi, wakati Barca ikipendekeza kutovuka euro milioni 5 kwa mwaka na kutomuhakikishia mkataba mrefu.
Lakini sasa, Bartomeu anaelezwa kuwa tayari kuongeza dau kuhakikisha anambakisha beki huyo veterani ambaye kubaki kwake ni muhimu kwa sababu Barca haiwezi kuchukua mchezaji mpya hadi Januari 2016.


Comments