KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema sasa malengo yake ni kushinda mechi mbili zijazo ili kutwaa kombe lake la Kwanza Tanzania.
Pluijm anayewakosa wachezaji muhimu kwasasa kutokana na majeruhi wakiwemo Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Salum Telela amesema yeye hazungumzii wachezaji majeruhi bali anazungumzia wachezaji waliopo.
"Timu hii inawachezaji wengi, wote ni wazuri na unaweza kuwatumia wakati wowote. Leo (jana) nimewakosa Cannavaro, Yondan, Telela, lakini Saidi (Juma), Zahir (Rajabu), Mbuyu (Twite) wameziba mapengo hayo na kupata ushindi". Amesema Pluijm.
Kuhusu kumuweka benchi goli kipa Ali Mustafa 'Bartez', Pluijm amesema yeye hana wasiwasi na uwezo wa makipa wake.
"Naamini Yanga ina makipa wazuri, 'Dida (Deo Munishi) na kipa mzuri sawa na Bartez (Ali Mustafa), kutokana na ubora wao nimeamua leo nimpumzishe Bartez ili Dida acheze. Ni sababu za kimpira tu wala hakuna kingine" Amesema Pluijm.
Kuhusu Andrey Coutinho Pluijm amesema: "Kwa muda mrefu amekaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi, lakini sasa ameimarika ingawa si kwa asilimia 100, kicuhezaji anahitaji mechi angalau mbili zao ili kurudi kwenye kiwango chake".
Comments
Post a Comment