PEP GUARDIOLA ASEMA KIPIGO CHA BORUSSIA DORTMUND HAKIWAVUNJI MOYO KUELEKEA NUSU FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE



PEP GUARDIOLA ASEMA KIPIGO CHA BORUSSIA DORTMUND HAKIWAVUNJI MOYO KUELEKEA NUSU FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE
Bayern Munich coach            Pep Guardiola was back at Bayern Munich training with a smile            on his face

Pep Guardiola amesema kipigo walichopata dhidi ya Borussia Dortmund katika nusu fainali ya Kombe la Ujerumani â€" DFB Pokal akimaanishi chochote kuelekea mechi yao ya nusu fainali ya Champions League dhidi ya Barcelona.
Kocha huyo amekataa kuwalaumu wachezaji wake baada ya kushuhudia wakipoteza mechi hiyo kwa penalti usiku wa Jumanne na kuwataka wasione aibu kwa kipigo hicho.
Pierre-Emerick Aubameyang alifunga dakika ya 75 kusawazisha bao la Robert Lewandowski na kuupeleka mchezo dakika za nyongeza ambazo hazikutoa mshindi na kwenye mikwaju ya penalti, Bayern walikosa nne wakati Ilkay Gundogan na Sebastian Kehl waliifungia BVB.

“Nina fahari na timu yangu. Kwa kweli sijawahi kuwa na fahari hii ya wachezaji wangu. Tulicheza vizuri sana. Ulikuwa ni mchezo bora tuliocheza dhidi ya Dortmund tangu nilipowasili Bayern,” alisema Guardiola kuiambia Sky.
“Hiki si kitu cha aibu. Tumepoteza mechi ya soka. Kuona aibu kunahitaji kuwapo kitu kibaya. Hii haina maana yoyote kwa mchezo dhidi ya Barcelona. Hiyo ni mechi mpya na ushindani mpya.”


Comments