Pep Guardiola amesema atabaki Bayern Munich msimu ujao licha ya klabu hiyo ya Bundesliga kuwa na wiki mbaya katika Champions League.
"Bila shaka nitakaa hapa msimu ujao," alisema na kuongeza kuwa yu tayari kupambana na changamoto.
Bayern ilikubali kichapo cha mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Champions League nyumbani kwa FC Porto, huku daktari wa timu akibwaga manyanga akisema kikosi chake cha matabibu kinastahili kuwajibika kwa kipigo hicho.
Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt, ambayeb pia ni daktari wa timu ya taifa ya Ujerumani kwa miaka mingi, amesema katika taarifa yake kuwa "uhusiano wa kuaminiana umeharibika" wakati yeye na wasaidizi wake watatu wakitangaza kuachia ngazi.
Bayern iliwakosa wachezaji wake watano muhimu kutokana na majeruhi katika kipigo hicho ambao ni Franck Ribery, Arjen Robben, David Alaba, Bastian Schweinsteiger na Javi Martinez.
Inaaminika Guardiola hajapendezwa na kazi ya Dk. Muller-Wohlfahrt ingawa hajamnyoshea kidole cha lawama hadharani.

Comments
Post a Comment