PATRICE EVRA AJIPANGA KUWA KOCHA, ASEMA NI USHAURI WA SIR ALEX FERGUSON



PATRICE EVRA AJIPANGA KUWA KOCHA, ASEMA NI USHAURI WA SIR ALEX FERGUSON

Beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra amefichua kuwa Sir Alex Ferguson alimwambia atakuja kuwa kocha mkubwa pamoja na Ryan Giggs.
Evra aliondoka Man United na kujiunga na Juventus kiangazi kilichopita, wakati Giggs alikuwa kocha wa muda Old Trafford mwaka uliopita kabla ya kuwa msaidizi wa Louis van Gaal.
Beki huyo wa kushoto amesema anachukua mafunzo ya ukocha baada ya kupata Baraka za Ferguson kabla hajastaafu.
"Ni hisia ngeni zilizokuja ambazo awali sikuwa nazo. Kabla Ferguson kustaafu aliniita ofisini kwake.
 "Aliniambia 'Pat, nitakwambia kitu muhimu sana. Kuna wachezaji wawili ambao watakuwa makocha wakubwa katika timu hii. Hao ni  Ryan Giggs na wewe.'
"Nimefuzu baadhi ya mafunzo yangu ya ukocha Manchester. Nimefanya mambo yote haya kimyakimya. Nataka kufaulu mafunzo haya ya ukocha na baada ya hapo tutaona," alisema.


Comments