Mlinzi wa hoteli ya Chelsea alimpagawisha Jose Mourinho kabla ya mechi ya Premier League dhidi ya Manchester United baada ya kuchanganywa na kaka wa kiungo wa wapinzani wao hao, Marouane Fellaini.
Baada ya kumuona kaka huyo ambaye ni pacha wa Fellaini mlinzi huyo alidhani kwamba kiungo huyo wa United hatacheza mechi hiyo.
Si tu Fellaini angecheza mechi hiyo, lakini pia alitarajiwa kuwa nguzo kuu ya United katika mipango yake, na ndiyo maana mwandishi wa gazeti la Dailly Mirror, John Cross aliripoti kuwa Mourinho alikuwa akihangaika wiki yote kabla ya mechi jinsi ya kumdhibiti nyota huyo.
Kaka huyo wa Fellaini – anayefanana na mdogo wake karibu kila kitu, hadi mtindo wa nywele, alionekana katika hoteli hiyo kabla ya mechi hiyo kubwa.
Wakati huo Mourinho alishamwandaa mtu maalumu - Kurt Zouma - kwaajili ya kuhakikisha Fellaini hafurukuti uwanjani na hivyo kitendo cha kuambiwa Mbelgiji huyo hata cheza kilimchanganya.
Kwa mujibu wa Cross, Mourinho alisema: "Nilikuja chini asubuhi na mlinzi akasema 'Fellaini hachezi'. Mlinzi alimuuliza 'unataka nini hapa?'. Akajibu 'mimi ni Fellaini na nimekuja kuchukua tiketi kwa rafiki yangu Eden Hazard."
Cross anasema habari hiyo ilimshtua Mourinho ambaye harakaharaka alichukua simu yake na kuingia kwenye mtandao wa Google na kumtafuta kaka wa Fellaini ambaye alionekana kufanana sana na nduguye.
Mansour Fellaini (kushoto) pacha wa MarouaneFellaini akipozi na kaka yake enzi zake za kuitumikia Everton kabla ya kujiunga na Manchester United
Baada ya kupata picha hiyo, Mourinho alitafuta na ya Fellaini mwenyewe akamuonyesha mlinzi zote mbili na kumuuliza, "ni huyu au huyu?" Mlinzi yule aliziangalia kisha akajibu "huyu". Alikuwa kaka mtu, Mourinho akapumua.
Comments
Post a Comment