Okwi, Busungu watambiana Simba ikipepetana na Mgambo



Okwi, Busungu watambiana Simba ikipepetana na Mgambo
s4
SIMBA SC inamtumia kiungo wake mshambuliaji Emmanuel Okwi katika mechi ya leo ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa  uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya Mgambo JKT.
Mechi ya kwanza iliyopigwa Mkwakwani, Mgambo walishinda magoli 2-0.
Simba wanaingia uwanjani wakiwa na machungu ya kuchapwa 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa mwishoni mwa juma lililopita uwanja wa Sokoine, Mjini Mbeya.
Kuelekea katika mpambano huo, Okwi aliyeikosa mechi iliyopita kwa kuwa na kadi tatu za njano amesema atajitahidi kuisaidia timu yake ipate matokeo.
"Namshukuru Mungu tuko salama, mimi na wachezaji wenzangu tuko katika morali kubwa. Tulipoteza mechi Mbeya, hatujakata tamaa, leo tunapambana kupata pointi tatu". Amesema Okwi.
Wakati Okwi akiwa na matarajio ya kupata ushindi, naye mshambuliaji nyota wa Mgambo JKT, Malimi Busungu ambeya anawaniwa na Simba, Yanga amesema leo ni siku nyingine ya kuonesha uwezo wangu.
"Hii ni mechi yangu muhimu kuwaonesha tena watanzania uwezo wangu, nitapambana na kuhakikisha nakuwa chachu ya ushindi, cha msingi dhuluma isiwepo, mechi hizi za mwisho zina mambo yake".


Comments