YANGA SC inaweza kutawazwa mabingwa kesho uwanja wa Taifa kama watashinda mechi yao dhidi ya Polisi Morogoro.
Mechi ya kesho ni muhimu kwa Yanga kuvuna pointi tatu na kama watafanikiwa basi watafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote na wakatakuwa wametwaa kombe kabla ya mechi mbili za mwisho.
Haruna Niyonzima, kiungo fundi ligi kuu amesema kwamba wanamejiandaa kufanya kazi nzuri na kuchukua ubingwa kabla ya kwenda Tunisia kucheza na Etoile du Sahel, mechi ya marudiano hatua ya 16 bora na mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa.
"Sisi sahizi ni kulazimisha, uwe umebana umeachia lazima tushinde, kesho Polisi lazima tuwafunge na kutangaza ubingwa".
"Tunamshukuru Mungu timu iko katika morali na kesho tutaendeleza furaha kwa mashabiki wetu". Amesema Niyonzima.
Comments
Post a Comment