Tattoo aliyochora Ngassa mkononi
'Katika siku za karibuni Ngassa alikuwa hashangilii magoli anayofunga Yanga, jambo lililotafsiriwa ni ishara ya kuichoka klabu hiyo ya Jangwani.'
WINGA hatari wa Yanga SCD na Taifa Stars, Mrisho Ngassa, ameanzisha mtindo mpya katika maisha yake ya soka kwa kumbusu mke wake pale anapofunga goli.
Katika mechi iliyopita waliyoshinda kwa mbinde nyumbgani 3-2 dhidi ya Stand United FC ya Shinyanga katika Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumanne, Ngassa alishangilia kwa kubusu mkono wake wa kushoto baada ya kufunga bao la pili.
Ngassa ndiyo mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kujibusu kwenye tattoo zake kila anapofunga bao alifanya hivyo kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana mjini Lobatse, ushangiliaji ambao unafanana na ule wa mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez.
Je kama atafunga leo atashingilia hivyo tena? tusubiri…..
Comments
Post a Comment