Ndoa ya mastaa wa Bongo Movies, Michael Sangu          'Mike' na Salome Urassa 'Thea' inadaiwa kuanguka chali kwa mara          nyingine baada ya mwanadada huyo kurudi kwa wazazi wake kwa muda          mrefu sasa.Chanzo makini kilidai kwamba, wawili hao walitengana          miezi mitatu iliyopita na Thea kurudi nyumbani kwa mama yake          maeneo ya Kinondoni jijini Dar kutokana na kile kilichodaiwa          kuwa ni migogoro ya mara kwa mara.                    Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu waliwaendea          hewani kwa nyakati tofauti, Mike na Thea ambapo kila mmoja          alifunguka kivyake. "Mh nani kawaambia maneno hayo? Watu          wanapenda kuzusha sana, mimi najua mke wangu bado nipo naye          amekwenda kwao kupumzika atarudi," alisema Mike.
Kwa upande wake Thea alifunguka: "Mmh, hakuna kitu kama hicho nani aliyewaambia, Mike kama amesema nimeenda kupumzika anajua yeye, kwanza naenda kupumzika nina mimba? Mimi nilikuwa 'production' na hivi ndiyo narudi nyumbani nikifika nitakupa simu uongee na Mike."Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni Thea hakuwasiliana na mwandishi ambaye anasubiri simu yake mpaka sasa.

Comments
Post a Comment