Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure ameripotiwa kukubaliana suala la malipo binafsi na klabu ya Inter Milan ya Italia kuelekea kukamilisha dili la uhamisho wenye thamani ya pauni milioni 5.7 kiangazi hiki.
Baada ya kiwango chake kuporomoka, mustakabali wa Toure ndani ya Etihad umekuwa na shaka wakati City ikionekana kutaka kukikwamua kikosi kwa kuwaacha wachezaji wenye umri mkubwa na kujaza vijana wa Kiingereza wenye kipaji.
Uwepo wa Roberto Mancini katika klabu ya Inter unaelezwa kuweka uwezekano mkubwa wa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast kuondoka City, na kwa mujibu wa Sportsmediaset tayari amekubali mkataba wa miaka minne wenye thamani ya karibu pauni milioni 12.8 ili kuichezea klabu hiyo ya Serie A.
Inter imeripotiwa kuilipa City pauni milioni 5.7 na bonasi kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 kama ataisaidia kupata tiketi ya kucheza Champions League msimu ujao.
Comments
Post a Comment