MAKALA HII NI KUTOKANA NA MAZUNGUMZO YANGU NA PAUL GAMA MIAKA MIWILI ILIYOPITA.PAUL AMEFARIKI DODOMA TAREHE 16 APRIL 2015, SAA NNE ASUBUHI. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI
| Paul Daniel Gama | 
Paul                Daniel Gama alizaliwa Barabara ya 11 Dodoma (1947). Baba                yake alikuwa ni
mwanajeshi wa KAR mwenye asili ya Songea na mama yake alikuwa na asili ya
Usangu alikuwa anafanya kazi katika
          mwanajeshi wa KAR mwenye asili ya Songea na mama yake alikuwa na asili ya
Usangu alikuwa anafanya kazi katika
|  | 
| Spokes Mashiyane na filimbi yake | 
hospitali                ya Mirembe ambayo wakati huo ilikuwa ni hospitali kubwaya                majeruhi wa vita ya pili ya dunia. Aliingia shule na                alipofika darasa la
nne alijikuta akiwa na kipaji kIkubwa cha kupiga filimbi, wakati huo wapigafilimbi walipenda sana kumuiga mpiga filimbi maarufu kutoka Africa ya Kusini Spokes Mashiyane. Akiwa na wenzie walianzisha kikundi ambacho kilikuwa na
maskani eneo la Mji Mpya pale Dodoma. Vijana hao pia walikuwa wakiiga nyimbo za wanamuziki maarufu wa wakatihuo, kama Salum Abdallah na CubanMarimba, pia Salum Zahor na Kiko Kids. Katika kufanya fani yao hiyo kama kitu cha kujipa burudani waliligusa sikio la aliyekuwa mwalimu wa Elimu ya Watu Wazima katika Community Center ya pale Dodoma. Mwalimu huyu aliwasaidia kuwaazimia amplifaya moja kutoka kwenye bendi nyingine ilikuweko Dodoma wakati huo, The Jolly Sextet Band. Band
iliyokuwa ikimilikiwa na Mkenya mmoja ambaye alifika Dodoma kama mfanya kazi wa
East African Postal and Telecommunication Services, huyu bwana alikuja na vyombo vingi akaanzisha bendi ambayo mmoja wa wapigaji wake alikuwa Mzee Mnenge ambaye hatimaye alitua NUTA Jazz Band.

| Bongos | 
Hiki kikundi cha Gama na wenzie                kilikuwa katika mfumo wa Jazz Band za zamani ambapo                walikuwa na ngoma na filimbi tu,ikisindikizwa na kuimba,                lakini waliweza kukonga nyoyo hata za wanamuziki wengine,                na Gama akawa anasakwa na bendi kubwa iliyokuweko wakati                ule Central Jazz band. Alipomaliza darasa la saba tu ndugu                yake aliyeitwa Titus Olaf Gama alimshawishi aingie Central                Jazz lakini hakuwa tena mpiga filimbi bali mpiga Bongos,                fani aliyoiweza sana hata  kuipenda na hasa baada ya                kuwaona wanamuziki wa NUTA akiwemo Muhidin Gurumo ambaye                wakati huo alikuwa akipiga Bongos na kuimba. Bongos no                ngoma ndogo zilizokuwa muhimu katika kundi wakati huo                ambapo hakukuweko na drums wala tumba. Taratibu akaanza                kupata hamu ya kupiga bass, wanamuziki wenzie walimkatisha                sana tamaa kwa kuambiwa kuwa vidole vyake vilifaa sana kwa                kupiga bongos na si kupiga gitaa. Katika jitihada                zake za kujifunza gitaa la bezi alikuwa kila mara akiwahi                mazoezi na kujaribu kujifunza gitaa la bezi. Hilo lilikuwa                gumu mpaka pale bendi  ya Lake Jazz Band ilipotembelea                Dodoma.
Bendi hiyo wakati huo ikiwa na wanamuziki kama Shem Karenga akiwa anapiga gitaa la bezi, Mzee Salum ambaye alikuwa na ulemavu wa macho, mwanzo alikuwa akipiga gitaa la solo na baadae akahamia kupiga gitaa la rhythm wakati gitaa solo lilikuja kupigwa na jamaa aliyeitwa Kally. Kutokana na simulizi ni wazi kuwa wanamuziki wa kutoka Burundi walikuwa wengi sana nchini wakati huo. Pia katika bendi hiyo alikuweko Mzee Juma Kitambi, mtunzi wa wimbo maarufu wa Rangi ya Chungwa. Gama alichukua nafasi hii kumfuata Mzee Salum ili aweze kumfundisha gitaa. Kwa kuwa wanamuziki wengine walikuwa wakitoka kwenda kutembea Mzee Salum alibakinyumbani na hivyo Gama alichukua nafasi hiyo kumnunulia sigara Mzee Salum anakumsihi amfundishe gitaa nae alifanya hivyo na Gama akatokea kuwa mpiga bezi mahiri.

Katikakipindi hiki akatokea                  mfanya biashara Mohamed Omar Badwel, huyu alikuwa                  nagereji na studio ya kupiga picha, aliweza kwenda                  Mombasa na kurudi na seti ya vyombo na kuanzisha Dodoma                  Jazz Band. Gama akahama Central Jazz Band nakujiunga na                  wanamuziki wengine walioanzisha Dodoma Jazz. Band                  ilianza ikiwa nampiga solo Hassan Mursali mwanamuziki                  mweny asili ya Malawi, siku hizo ikiitwa Nyasaland                  alikuwa ndie mpiga solo, lakini aliwaacha baadae na                  kujiunga na NUTA Jazz Band, upigaji wake wa solo unaweza                  kuusikia katika kusikiliza kibao kimoja maarufu cha                  NUTA, kilichoitwa Dunia Njema Kukaa Wawili. Hasan                  alikuwa mtu wa kuhama hama hatimae alipoteza uwezo wa                  kusikia jambo ambalo lilihusishwa na kuhamham kwake                  kwani ushirikina ulitawala sana wakati huo, kama maelezo                  yanayofuata yanavyoonyesha. Dodoma Jazz ilikuwa pia                  inafanya ziara katika sehemu nyingi, kama vile Iringa,                  Mbeya ,Tabora, Dar es Salaam na kadhalika, lakini safari                  moja ya kwenda Kilosa ilifanyika ikiwa na lengo la                  kumfuata Abel Barthazal aliyekuwa akipiga katika bendi                  ya Kilosa Jazz.
Bendi ilipokelewa vizuri na wakafanya maonyesho yao Kilosa na hatimae kuondoka na Abel. Siku chache baade wakati huo Mzee Mohamed Omar, mwenye bendi alikuwa kasha mnunulia suti kadhaa Abel, ukaja ugeni toka Kilosa wakiwa na barua yenye maelezo kuwa ikiwa Abel Hatarudi Kilosa, mmoja wa wanamuziki wa Dodoma Jazz atafariki, na barua hii ililetwa kwa mkono na mjumbe ambae alisisitiza wakishaisoma mbele yake ndio anaondoka. Abel alirudishwa Kilosa mara moja.

Baada ya hapo aliyekuwa meneja wa                  bendi Ramadhan Waziri alitumwa Burundi kwenda kutafuta                  wapigaji, siku alipokuwa anarudi na wapigaji wapya                  akakutana kwenye treni na Rashid Hanzuruni, mpiga solo                  mahiri sana ambaye upigaji wake husikika katika wimbo                   Napenda nipate lau nafasi
            Hanzuruni alikuwa kaiacha Tabora                  Jazz baada ya kutokea ugomvi mkubwa ambapo alipoteza                  meno kadhaa, hivyo alikuwa kwenye hilo treni akielekea                  Dar es Salaam kumfuata mpigaji mwenzie Samba ambae                  alikuwa NUTA Jazz. Ramadhani aliweza kumshawishi                  hanzuruni akabaki Dodoma Jazz ambako
alikaa kwa muda na hatimae akaja kuchukuliwa na Sama ili aingie NUTA Jazz, ndoto hiyo haikufanikiwa kwana NUTA alikuweko mpigaji mahiri Hamisi Franco, hii ndiyo ilipelekea Hanzuruni kwenda Western Jazz Band

Comments
Post a Comment