MWANAMUZIKI mkongwe Willie Nelson ametangaza kuanza kuuza bangi yenye label yake. Willie ambae ana umri wa miaka 81 amesema anataka kuuza bangi ambayo itakuwa na ubora wa hali ya juu kuliko bangi nyingine iliyoko sokoni. Bangi hiyo ambayo amesema itaingia sokoni ikiwa na jina la Willie Weed, itasambazwa na kampuni yake mpya inayoitwa Willie's Reserve. Bangi hiyo itakuwa inapatikana Colorado and Washington (USA) ambako bangi imeruhusiwa kwa matumizi ya burudani. Akiwa anahojiwa na gazeti maarufu la Rolling Stone, Willie alisema kuwa atahakikisha anafanya kazi bega kwa bega na wakulima wa bangi ili aweze kupata bangi bora . Willie sio mwanamuziki wa kwanza kuanza biashara ya bangi pia rapa maarufu Snoop Dog nae kawekeza kwenye bangi iliyopewa label ya Eaze.
Comments
Post a Comment