Mtibwa Sugar yadundwa nyumbani


Mtibwa Sugar yadundwa nyumbani
mtibwa-sugar
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mtibwa na JKT Ruvu zilitoka sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya VPL msimu huu iliyochezwa Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam.'
MABINGWA wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar FC, wamepoteza mechi yao ya kwanza nyumbani msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro baada ya leo kupigwa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu  Stars. 
Bao pekee la kujifunga la beki wa kati Andrew Vincent, limetosha kukisogeza kwa nafasi moja kikosi cha Fred Felix Minziro kutoka nafasi ya 11 hadi ya 10 katika msimamo wa ligi kikiishusha Coastal Union FC kwa nafasi moja.
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar FC, mzawa Mecky Mexime, aliyewahi kuwa nahodha wa Taifa Stars na Mtibwa katika enzi zake za kusakata soka, amesema baada ya mechi kuwa ubora wa kipa wapinzani wao aliyeokoa mashuti mengi ya wenyeji.
Mtibwa wameendelea kubaki nafasi ya saba katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 28 sawa na Stand United, Mgambo Shooting, JKT Ruvu na Coastal Uniuon zinazokamata nafasi za 8-11.


Comments