MASHABIKI WA TAARAB WALIVYOJINOMA KWA MUZIKI WA JAHAZI DAR LIVE



MASHABIKI WA TAARAB WALIVYOJINOMA KWA MUZIKI WA JAHAZI DAR LIVE

Pata picha kadhaa za onyesho la Jahazi Modern Taarab lililofanyika Dar Live Jumamosi iliyopita.
Lilikuwa ni onyesho maalum la Mfalme Mzee Yussuf kutimiza miaka 11 ya uimbaji wa taarab, tukio lilibatizwa jina la "Usiku wa Mfalme" huku likichagizwa na kauli mbiu iliyosema Mwacheni Mfalme aitwe Mfalme.
Ama Kwa hakika lilikuwa ni onyesho la aina yake lililoacha historia ya aina yake ambapo Mzee Yussuf alipiga aina ya show itakayoendelea kubakia kuwa kumbukumbu nzuri katika maktaba ya matukio ya taarab.
Mashabiki wakiserebuka huku wakiwa na picha ya Mzee Yusuf.
Leila Rashid akipagawisha mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka kwa raha zao.
Shabiki (aliyeinama) akionyesha kipaji cha kukata viuno.
Wanenguaji wa Jahazi wakipozi mbele ya kamera.
Shabiki akimtunza pesa Hadija Yusuf.
Musa Musa akilicharaza gitaa.
 
Shabiki aliyetaka kuingia bure ukumbini baada ya kutaitiwa na walinzi.
Fatma Kassim akiimba.
(Habari na Saluti5, PICHA ZOTE NA GLOBAL PUBLISHERS) 


Comments