MARA MWISHO LIVERPOOL WAMESHINDA TAJI LA EPL…COUNTINHO,STERLING WALIKUA HAWAJAZALIWA…SOMA FACT NYINGINE



MARA MWISHO LIVERPOOL WAMESHINDA TAJI LA EPL…COUNTINHO,STERLING WALIKUA HAWAJAZALIWA…SOMA FACT NYINGINE

LIVERRRRRRRRRRRR

Mara ya mwisho Liverpool inashinda ubingwa wa ligi ya england wachezaji kama Phillipe Countinho, Jon Flanagan,Jordan Henderson,Raheem Sterling walikua bado hawajazaliwa.

Tangu amshabiki wa Liverpool washangilie ubingwa wa ligi zimepita siku 8750, maana yake ni kwamba kuna asilimia kubwa ya mashabiki wa Liverpool hawajawai kusherekea ubingwa wa EPL.

Kwa muda wote huo wamekua na manager 8,wametumia zaidi ya Pound milioni 650 kwenye uhamisho wa wachezaji na baadhi yao ni Luis Suarez Pound milioni 23, Torres Pound million 26.5,Xavi Alonso Pound milioni 10.5,Stewart Downing Pound milioni 20, Andy Carrol Pound millioni 35, Alberto Aqualiani Pound millioni 17.

Tangu wakati huo Manchester wameshinda titles 13, Arsenal mara 4 ,Chelsea mara 3, Leeds, Blackburn na Man City wameshinda mara 1.

Katika muda huo huo wa miaka hiyo yote Giggs amebadilisha professional kutoka mchezaji hadi kocha, kacheza mechi 1000,kashinda magoli 181 na kushinda mataji 35

Pia katika muda huo huo Jose Mourinho amekua kocha, amefundisha timu 6, ameshinda mataji makubwa 20 yakiwemo mawili ya EPL ambalo Liverpool halijalionja miaka mingi iliyopita.

Katika huo huo muda ticket za kuangalia mechi ya Liverpool imepanda kwa asilimia 1031. Mfano kutoka msimu wa 1989/90 bei ilikua pound 65 lakini sasa hivi ni pound 735



Comments