Manchester United imeanza kusaka mbadala wa muda mrefu wa Michael Carrick ambapo Ilkay Gundogan (pichani) anaonekana kuwa chaguo kuu.
Kocha Louis van Gaal amekuwa akivutiwa sana na machango wa Carrick Old Trafford msimu huu.
Pasi za uhakika za mchezaji huyo wa kimataifa wa England pamoja uwezo wake wa kuudhibiti mchezo, umemfanya awe nguzo muhimu ya United.
Lakini kwa umri wake wa miaka 33 unamfanya Van Gaal atambue kuwa kiungo wake anaelekea ukingoni huku majereha ya mara kwa mara ya Carrick nayo yamekuwa yakileta hofu Old Trafford.
Na sasa Van Gaal anamtazama Ilkay Gundogan Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 24 kama suluhisho halisi la safu yake ya kiungo.
Comments
Post a Comment