MANCHESTER UNITED YAHESABU SIKU KUMNASA MEMPHIS DEPAY WA PSV …usajili wa pauni mil 25 waelekea kukamilika



MANCHESTER UNITED YAHESABU SIKU KUMNASA MEMPHIS DEPAY WA PSV …usajili wa pauni mil 25 waelekea kukamilika
Manchester            United have made an official approach for Memphis Depay            (right), says PSV's technical director

Manchester United inakaribia kumnasa winga wa kimataifa wa Holland na PSV Eindhoven, Memphis Depay (pichani kulia).

PSV imethibitisha kuwa Depay anategemewa kuondoka mwishoni mwa msimu na inaaminika kuwa vilabu hivyo viwili viko kwenye maongezi juu ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye anachukuliwa kama mmoja wa wanasoka mwenye kipaji cha hali ya juu barani Ulaya.

Dapay alifunga kwa free kick ya aina yake kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Heerenveen Jumamosi iliyopita na kuisaidia PSV kutwaa ubingwa wa Holland kwa mara ya kwanza toka mwaka 2008.

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal alisafiri hadi Amsterdam kwenda kumwangalia Depay mwezi uliopita wakati Holland ilipocheza mechi ya kirafiki na Hispania na kuibuka na ushindi wa 2-0.

United ipo kwenye nafasi nzuri ya kuthibitisha kumtwaa Depay kwa pauni milioni 25 na kuipiku Paris St-Germain ambayo nayo imekuwa ikihusishwa na winga huyo.

Mkurugenzi wa PSV Marcel Brands amesema kuna ofa kutoka klabu kubwa za Ulaya na pindi watakapofikia muafaka watamwacha Depay achague mwenyewe pa kwenda. "Itakuwa ni vigumu kwetu kusema hapana  kwa aina hii ya klabu tuliyonayo," alisema Brands.



Comments