MANCHESTER UNITED USO KWA USO NA LIVERPOOL RADJA NAINGGOLAN WA AS ROMA



MANCHESTER UNITED USO KWA USO NA LIVERPOOL RADJA NAINGGOLAN WA AS ROMA

Manchester United imeripotiwa kuingilia mipango ya Liverpool kwa kutaka kuweka mezani pauni milioni 29 kumsajili kiungo Mbelgiji anayekipiga AS Roma ya Italia, Radja Nainggolan (Pichani juu) baada ya kumfuatilia katika mechi ya karibuni.
Nainggolan – anayemilikiwa kwa pamoja na AS Roma na Cagliari – anaelezwa kujiandaa kuhama mwisho wa msimu kutokana na Roma kutoweza kumpa mkataba wa kudumu.
Liverpool inaelezwa kuwa na matumaini ya kumpeleka staa huyo Anfield, lakini kwa mujibu wa gazeti la Corriere dello Sport Man United imeingilia dili lake baada ya kutuma maofisa wake kwenda kuweka mambo sawa.


Comments