MAMBO MATANO AMBAYO BARCELONA INAPASWA KUFANYA ILI KUIFUNGA BAYERN


MAMBO MATANO AMBAYO BARCELONA INAPASWA KUFANYA ILI KUIFUNGA BAYERN

luis-suarez-messi-and-neymar-in-fc-barcelona-2014-2015

1. Kuzuia hatari zozote zitokanazo na adhabu ndogo (set pieces). Tumeona msimu huu kumekuwa na magoli machache yalotokana na uzembe. Katika msimu huu Barcelona imeweza kuwa na clean sheets 28 katika mechi 51 ambayo ni 54% kulinganisha na misimu mingine ambayo Barca iliweza kuwa na clean sheets. Rekodi ilioko inaonesha kuwa msimu wa 1986-87 ndio unaokaribia kwa kuwa asilimia 53% (yaani mechi 54 na kuwa na clean sheets 29). Ili kuimarisha uwezo wa kuongeza clean sheets Barcelona inapaswa kuepuka makosa yasio ya lizima katka eneo la nje ya 18 'avoiding unnecessary free kicks'.

  1. Kucheza kwa umakini, mtu na mtu, (Zonal marking). Kila mchezaji atoe mchango 120% ili kuhakikisha kunakuwa na team balance, mabeki wa pembeni wazime mashambulizi ya kushtukiza na kuhakikisha kuwa kama ni kupanda mbele na kurudi nyuma kutengeneza 'balance' uwiano. Jordi Alba ni mzuri zaidi katika hilo.
  2. Kuendelea kushambulia pasipo kuridhika na goli1 au mawili. Hapa naona kuna haja ya Enrique kufanyia kazi maana kama ni kikosi cha kwanza amepata. Kuna mifano kadhaa tumeona mpaka sasa kuwa timu imekuwa ikicheza kwa kuridhika hasa baada ya kuwa imeongoza. Mfano mzuri ni ile mechi ya ManCity vs Barcelona na ile ya Sevila vs Barcelona hivi karibuni ambapo tulishuhudia udhaifu huo.
  3. Kucheza kwa kasi na kupiga pasi zenye macho. (Moving the ball quickly). Kama kupoza mpira ili kufisha mashambulizi ya timu pinzani ambapo Xavi Hernandez ('The living legend') ni mtaalam katika hili, ni muhimu sana kufanya hivyo na kuepuka kupoteza mipira kirahisi hasa katika eneo la katikati na hivyo kuzuia kaunta (mashambulizi ya kustukiza) ambayo yangeweza kuepukika.
  4. Kutumia nafasi vizuri, (to be clinical in finishing) na kuwa na ubunifu wa ziada kwa kupiga nje ya box. Kumiliki mpira ni jambo moja ila kutengenza nafasi na kuitumia ni jambo lingine. Lazima tukubali kubadilika, timu iburudishe ila itumie nafasi kila inapopatikana. Mara zote ambapo Neymar na Suarez walipotimiza wajibu wao vema tumeona magoli yakipatikana.

KILA LA HERI BARCELONA, Visca el Barca!!

  • Itaendelea wiki ijayo ambapo tutazungumzia ubora na udhaifu wa Bayern. Uchambuzi wa mchezaji mmoja mmoja (wachezaji wa FC Barcelona na wale FCBayern.) (FCB vs FCB). Yote ni katika kuona wajibu wa kila mchezaji uwanjani.


Comments