Makata ajifananisha na daktari aliyepokea mgonjwa mahututi


Makata ajifananisha na daktari aliyepokea mgonjwa mahututi

Makata-e1425655002516

Mbwana Makata (wa kwanza kulia) akiiongoza timu yake kwa moja ya mechi za ligi kuu.

KOCHA mkuu wa Tanzania Prisons, Mbwana Makata bado hajakata tamaa ya kubaki ligi kuu licha ya timu yake kuwa dhoofu katika msimamo mpaka sasa.

Prisons ndio timu iliyofanya vibaya zaidi msimu huu ikiwa na pointi 22 mkiani baada ya kucheza mechi 23, lakini kocha wake (Makata) amesema: "Tuna mechi tatu ambazo zitaamua hatima yetu ya kubaki au kushuka daraja, niliichukua timu ikiwa mazingira magumu, lakini mimi kama mwalimu ni kama daktari, unamchukua mgonjwa ambaye yuko mahututi unajitahidi kuhakikisha unamponya. Ukiweza kuokoa maisha yake unaonekana bingwa na ukishindwa unaumia".

 

"Nitapambana sana, wanaojua mpira wa miguu wanajua nilichukua timu katika wakati gani, timu ilikuwa na pointi 11, kwahiyo atajua nilichokifanya, nitapambana kuhakikisha tunabaki".



Comments