MAGOLI 26 YA ALEXANDRE LACAZETTE YAMTIA WAZIMU ARSENE WENGER


MAGOLI 26 YA ALEXANDRE LACAZETTE YAMTIA WAZIMU ARSENE WENGER

Arsene Wenger yuko tayari kujaribu bahati yake kumsajili mpachika mabao nyota wa Lyon ya Ufaransa, Alexandre Lacazette.
Mabao 26 katika mechi 30 yamemwezesha Lacazette mwenye umri wa miaka 23 kuwa juu ya chati ya wafungaji katika Ligue 1 msimu huu, huku akiisaidia Lyon kulingana pointi kileleni na Paris Saint-Germian.
Ripoti ndani ya Italia zinapasha kuwa Wenger yu tayari lolote liwezekano kuhakikisha anamtia mikononi Lacazette kiangazi hiki ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.


Comments