Wazee wa mtonyo ambao waliwai kutoa picha yenye price tag ya wachezaji wakubwa kabisa na kusema kwamba wana mpango wa kuwaleta wote kwenye club ya Manchester city lakini haikua hivyo.
Hivi sasa wametenga dau la £30 million ili kujaribu kumpata star wa Arsenal mwenye miaka 23 Jack Wilshere. Gazeti la The Mirror limeripoti kwamba Manchester city wana plan hiyo kwa sasa japokua kwenye uhalisia Arsene Wenger hawezi kumruhusu mchezaji huyo kusepa.
Hivi sasa Wilshere ana mkataba na gunners hadi June 2018 ikimaanisha kwamba hayupo kwenye pressure yoyote ya kuhama hiyo club. The Mirror wanasema interest ya Man city kumleta Jack Wilshere Etihad inaweza kuwashawishi Arsenal kuingia kwenye mazungumzo hayo.
Mashabiki wa Arsenal wana wasiwasi kwasababu historia inaweza kujirudia kama ilivyotokea kwa Emmanuel Adebayor, Kolo Toure, Gael Clichy, Samir Nasri na Bacary Sagna ambao waliwai kuhama kutoka London kwenye Manchester.
Wilshere amekua majeruhi kwa muda mrefu na kumfanya atokee mara 9 tu kwenye msimu huu.
Comments
Post a Comment