LICHA YA KUTOLEWA NA MACHELA NA KUKIMBIZWA HOSPITAL, DAVID SILVA ASEMA YUKO FITI



LICHA YA KUTOLEWA NA MACHELA NA KUKIMBIZWA HOSPITAL, DAVID SILVA ASEMA YUKO FITI
Silva was taken off on a stretcher            before being rushed to hospital as Manuel Pellegrini has a            nervous wait 
David Silva amesema yuko fiti licha ya kuhofiwa kuvunjwa taya baada ya kupigwa kiwiko na Cheikhou Kouyate kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Ham.

David Silva (left) receives an            elbow to the face by the on-rushing Cheikhou Kouyate in the            second half

Nyota huyo wa Manchester City alitolewa kwa machela dakika ya nane huku akipewa msaada wa mashine za oxygen ili kumsaidia kupumua vizuri.

Silva was given put in a neck brace and given oxygen as              his concerned team-mates looked on

Alikimbizwa hospital na kuwaacha mashabiki wa timu yake wakiwa na wasiwasi juu ya afya yake lakini baadae kupitia mitandao ya kijamii, akatoa habari zilizoleta faraja.

"Shukrani nyingi kwa meseji zenu za kunitakia ahueni, vipimo vyote vimekwenda vizuri na tayari niko nyumbani. Pointi tatu zilizopatikana zilikuwa muhimu," aliandika kupitia Twitter. City ilishinda 2-0.

Mwamuzi Anthony Taylor  akamzawadia Kouyate kadi ya njano, baadae kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini akasema haamini kama kiungo huyo wa Senegal alidhamiria kumuumiza Silva.


Comments