Leo hatufanyi makosa, tunamaliza biashara mapema-Msuva


Leo hatufanyi makosa, tunamaliza biashara mapema-Msuva

msuva

SIMON msuva, winga hatari, mwenye kasi kubwa amesema leo anaandika historia ya kuchukua ubingwa kwa kufunga magoli mengi leo wakichuana na Polisi Morogoro uwanja wa Taifa.

Nyota huyo aliyefunga goli linaloelekeana na la Robin Van Persie kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil amesema amejiandaa vizuri kuongeza idadi ya magoli.

"Namshukuru Mungu nafanya vizuri msimu huu, naongoza kwa magoli 16, sijaridhika, napambana kufunga mengi zaidi". Amesema Msuva na kusisitiza: "Leo hatufanyi makosa, tunamaliza biashara mapema, naamini mashabiki wa Yanga watafurahia kazi nzuri tutakayofanya".



Comments