Kumbe ‘Ball Boys’ wanampenda Ivo Mapunda?


Kumbe 'Ball Boys' wanampenda Ivo Mapunda?

Taulo 3

IVO Mapunda ni miongoni mwa makipa waliopitia misukosuko mingi katika klabu za Simba na Yanga.

Kabla ya kuichezea Simba, Ivo alikuwa kipa mahiri ndani ya klabu ya Yanga na Taifa Stars, lakini alikuwa anatuhumiwa mara kadhaa kuihujumu timu na kushuka kiwango.

Ikafika wakati akaona isiwe taabu! akatimkia Ethiopia katika klabu ya Saint George na alicheza kwa mafanikio. Amepitia sehemu nyingi, lakini mwaka jana kabla ya kuja Simba alikuwa kipa muhimu kwenye kikosi cha Gor Mahia ya Kenya.

Kipa huyu ni mahiri kudaka penalti na kila ilipofikia hatua hiyo, Gor Mahia walimuingiza kuokoa jahazi na alifanya hivyo.

Aliposajiliwa na Simba amekuwa akicheza vizuri, kuna wakati anafanya makosa ya kimchezo, lakini watu wanazungumza vibaya.

Lakini cha kufurahisha ni kwamba Ivo kamwe hakati tamaa na muda wote anajituma, anajua kukubali changamoto na kupotezea maneno ya watu.

Jana aliidakia Simba baada ya kukosa mechi tatu kutokana na kupewa kadi nyekundu machi 18 mwaka huu Simba ikilala 2-0 dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.

Ilikosa mechi dhidi ya Ruvu Shootings Simba ikishinda 3-0, akakosa mechi na Kagera Sugar Mnyama akishinda 2-1 na mechi ya mwisho ni ile Simba waliyolala 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Taulo 1

Vijana wakikamua maji taulo la Ivo

Akiwa kwenye kiwango kikubwa, Ivo mwenye tabia ya kuwa na taulo kubwa golini jana alikumbwa na tatizo na nguo yake hiyo ya kufutia jasho ingawa wapinzani wanaitafsiri vibaya.

Taulo lilijaa maji, lakini vijana wanaookota mipira, 'Ball Boys' kwa mapenzi yao walilichukua taulo na kuanza kulikamua maji.

Walifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa na kumkabidhi Ivo, ilikuwa burudani nzuri sana.



Comments