Kocha Mgambo JKT ajibu mapigo kwa Simba



Kocha Mgambo JKT ajibu mapigo kwa Simba

1107922_heroa

SIMBA SC imetamba kumaliza hasira zake kwa Mgambo JKT katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara watakayokutana keshokutwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara alikaririwa na mtandao huu jana akikiri kuzidiwa na Mbeya City mechi iliyopita uwanja wa Sokoine na kufungwa 2-0, lakini akadai Mgambo waje vizuri kwani watamaliza hasira zao kwao.

Baada ya kusikia maneno hayo, kocha mkuu wa Mgambo JKT, Bakari Shime amejibu mapigo akisema walichokifanya Mkwakwani watakirudia tena uwanja wa Taifa.

"Walipokuja kwetu tuliwafunga 2-0, nilisema ukiangalia wachezaji wa Simba na Mgambo, sisi tuna uzoefu kuliko wao. Angalia mtoto kama Banda (Hassan) nimemfundisha mwenyewe, akina Mkude (Jonas), Ndemla (Said) nilikuwa nawafunga tu katika michuano ya vijana" Amesema Shime na kuongeza: "Kwa wachezaji kama hawa nitawaogopa? Mimi sijali Simba wala Yanga, naingia kutafuta pointi tatu, tutaonana uwanjani jumatano".



Comments