BAYERN Munich imeichapa mabao 6-1 FC Porto ya Ureno katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa ulaya iliyopigwa Allianz Arena, mjini Munich, Ujerumani.Watu wengi walifikiri Bayern anatoka kutokana na kipigo cha 3-1 walichovuna jumatano iliyopita, lakini walijidanganya licha ya timu hiyo kukosa baadhi ya wachezaji nyota.
Katika mechi hiyo ya marudiano ya robo fainali wenyeji hao walipata mabao yao kupitia kwa Thiago Alcantara, Robert Lewandowski aliyefunga mawili, Thomas Muller, Jerome Boateng na Xabi Alonso wakati wageni walipata bao pekee kutoka kwa Martnez.
maana yake munich wamefuzu kwa jumla ya mabao 7-4 dhidi ya wareno hao.
Comments
Post a Comment