YANGA SC imeshinda magoli            3-2 dhidi ya Stand United katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa            jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
        Magoli ya Yanga            yalifungwa na Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva kwa            mkwaju wa penalti.
        Baada ya kufunga goli            lake, Mrisho Ngassa hakushangilia kwa kawaida yake ya kwenda            kwenye kona ya kibendera, bali alionekana akibusu mkono wake.
        Mtandao huu ukadadisi,            kwanini Ngassa anabusu mkono wake na kuamua kumuuliza baada ya            mechi ana akajibu:
        "Nimebusu mkono            kwasabababu nimemchora 'Tattoo' mke wangu, mke wangu ndio kila            kitu, ndio mshauri wangu wa kila kitu, kwahiyo nikifunga goli            lazima nimbusu"
        Tattoo niliyochora ni            jina la mke wangu kwasababu nina mapenzo ya dhati kwake, yeye            ndiye mshauri wangu, anaitwa Nish Radhia"
        "Kuna tattoo nyingine            ambayo ni siri yangu pamoja na yeye, imechorwa kifuani"
        
Comments
Post a Comment