Zinedine Zidane alimsifia Gareth Bale kwamba ni mchezaji wa tofauti sana, baada ya summer kufika mwaka 2013 akahamia Real Madrid. Sasa wasiwasi umetanda kwa Hazard kuwa na uwezekano wa kuhamia Real baada ya Zidane kumsifia hivyo hivyo Hazard akimfananisha kama Cristiano na Messi kwa sasa.
Jose Mourinho akijibu kuhusu maneno ya Zidane alisema kwamba kama Real inamtaka Hazard, yeye (Mourinho) angekua wa kwanza kujua.Lakini kama ni kweli wanamtaka nay eye hajui basi itawagharimu £100 million kwa kila mguu wa Hazard.
Mourinho ambae leo ana mechi na Arsenal alisema kwamba haamini kama Real wanajaribu kum-sign Hazard kwasababu bado hawajamwambia. Uhusiano wake na rais wa timu na CEO hautoi nafasi ya kitu kama hicho kutoka nyumba ya mgongo wake. Lazima wangemwambia kwasababu wana aminiana kikamilifu.
Chochote kinaweza kutokea na Real Madrid kwenye kuweka mzigo mzito kumpata yule wamtakae, sio tatizo kubwa kwao. Tusubili tuone.
Comments
Post a Comment