Jerry Muro kuadhibiwa kwa kuingia na pombe uwanjani


Jerry Muro kuadhibiwa kwa kuingia na pombe uwanjani
Muro Mvinyo
'Muro amewahi kupewa onyo na TFF kutokana na maneno yake makali dhidi ya shirikisho hilo.'
MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jery Muro, yuko hatarini kuadhibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya jana kuingia na shampeni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kinyume cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014.
Muro alionekana akiwaongoza mashabiki wa Yanga SC waliokuwa wamefurika sehemu ya chini ya Jukwaa la VIP A kufungua shampeni mara tu baada ya timu yao kutwaa taji la 25 la Tanzania Bara ilipoinyanyasa Police Moro FC mabao 4-1.
Mshambuliaji wa zamani wa Vital'O ya Burundi na Simba na mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe, alipiga hat-trick yake ya pili msimu huu na kufikisha mabao 14, matatu nyuma ya kinara Simon Msuva wa Yanga SC pia.


Comments