Huu ndiyo ubovu wa ligi kuu Tanzania Bara 2014/2015



03

Na George Mganga

Kwanza na awali ya yote napenda kutoa shukrani na pongezi kwa wale wote mmekuwa karibu na mimi kusoma hizi makala ambazo nimekuwa nikiziandaa kwa hizi siku za karibuni.

Natoa pole na pongezi pia kwa Shirikisho na mpira wa miguu hapa nchini TFF kwa majukumu mazito na changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo katika kuhakikisha soka letu linasimama.

Tunajua TFF ndiyo kiongozi mkuu wa mpira hapa nchini na bila wao soka letu lisingekuwa hapa lilipo hivyo ni sawa kuwapongeza.

Ni mechi kadhaa sasa zimesalia kwa kila timu kumaliza idadi stahiki katika ligi kuu ya hapa Tanzania.

Na hapa tutajua ni timu zipi zitashuka daraja na zipi zitakuwepo katika michuano ya kimataifa na halikadhalika zitakazoshuka daraja.

Mengi zaidi tumeyashuhudia katika msimu huu ambayo yameshusha hata hadhi ya ligi yetu na yamekuwa yakirudisha zaidi maendeleo nyuma ya soka letu badala ya kwenda au kuendelea mbele zaidi.

Moja kati ya mambo ambayo hayaleti ubora na umakini wa ligi hii ni baadhi tu ya waamuzi ambao wamekuwa wakipigiwa kelele kila kukicha kwa tuhuma za maamuzi mabovu.

Waamuzi wengi tulionao hapa kwetu huwa hawawezi kabisa kuumudu mchezo kwa kwenda tofauti kabisa na maamuzi ya uwanjani ambayo huzingatia uwepo wa sheria 17 za soka.

Udhaifu huwa unakuja pale mwamuzi anapotoa kadi ovyo ovyo tu bila kuzingatia taaluma yake inapaswa afanye maamuzi gani pindi tukio la kimchezo linapotokea uwanjani.

Nadhani rushwa pia imekuwa ni sababu tosha inayosababisha haya yote kutokea kwani baadhi yao wamekuwa wakihongwa pesa ilimradi tu timu fulani iondoke na matokeo mabovu ili mwamuzi naye apate pesa yake.

Hili sio jambo dogo hata kidogo na inabidi TFF ichukue hatua pindi inapobainika mwamuzi kafanya jambo kama hili.

Kingine ni mvurugano wa ratiba na kupelekea mechi kubadilishwa tarehe mara kwa mara na naweza kusema tangu nianze kufuarilia soka la hapa kwetu sijawahi kuona ratiba ikibadilika mara kwa mara kiasi hiki.

Asili na asilimia kubwa ya timu zetu zimekuwa zikitegemea mapato ya viingilio vya milangoni na pesa inayopatikana ndiyo imekuwa ikiendesha timu hizo katika shughuli zote.

Fikiria timu kama Ndanda au Stand united imekuja hapa Dar es salaam kuweka kambi ya siku 4 na leo hii unawapa taarifa tena kwa kuwashtukiza tu kuwa mechi itachezwa siku 3 zijazo.

Moja kwa moja utakuwa umeshazitia hasara timu kama hizo ambazo hazijaimarika vizuri kiuchumi na badala yake utakuwa unazitia hasara tu.

Bodi ya ligi inajukumu la kujipanga tokea mwanzo pindi inapoandaa ratiba ya ligi kuu.

Inabidi tufikie wakati sasa wa kujaribu kuiga hata ligi za wenzetu sasa ili tuweze kuondoka katika hatua hizi tulizopo hivi sasa nantufike mbele zaidi katika soka letu.

Jambo lingine ni kuhusiana na maandalizi ya viwanja kuwa duni, ni malalamiko mengi sana yamekuwa yakitolewa na wachezaji pamoja na vilabu kuwa viwanja havina ubora.

Mfano mzuri ni kile kiwanja cha Mkwakwani Tanga kimekuwa kibovu sana siku zote na malalamiko yapo lukuki lakini hakuna hata urejesho wa kauli yoyote tokea TFF na wapo wanaona.

Timu mwenyeji siku zote hawezi kusema uwanja wake ni mbovu sababu ya uzoefu alivyozoea kuchezea hapo na hata mazoezi huwa anafanya lakini kwa timu ngeni huwa ni tatizo zaidi.

Timu mbili zenye jina kubwa hapa nchini zilishawahi kuulalamikia uwanja wa Mkwakwani kuwa haufai hata kuwa na hadhi ya kuuchezea sababu una kama mabonde kwenye pitch.

Naomba haya TFF iyaangalie kwa macho mawili makini zaidi ikiwepo na kufungia au kuzuia hivi viwanja vibovu au kupiga hata faini kwa vilabu husika hadi ukarabati utakapofanyika.

Gumzo kubwa ambalo lilitokea hapa katikati ya msimu wa ligi kubadilika kwa sheria ya mchezaji pindi anapopata kadi 3 za njano awe na fursa sasa ya kuchagua mechi ipi acheze.

Kwangu mimi naona ni maamuzi ambayo hayakuwa sawa kabisa kutokana na uamuzi wenyewe kuhusisha timu moja tu na vingine vikiwa havina taarifa sijajua hatima yake ilifikiaje baada ya uamuzi huo.

Ingekuwa vizuri zaidi kama chombo cha ligi kingekuwa kinandaa taarifa hizi mapema kufikisha katika timu zenyewe ili kuepusha malumbano ya kila siku.

TFF inapaswa kukaa na kujenga misingi mzuri katika kuendesha soka letu na kuwa na wajibu wakati wa kuandaa ratiba kila kitu kikishakamilika kusiwe na uhitaji wa mabadiliko mengine hapo baadae.

Hatuhitaji kuona ligi yetu inaenda kienyeji bali ni wakati sasa wa kuhakikisha tunaenda na wakati zaidi na sio tunarudi huko tulipotokea.

Ni halali yako kucomment chochote juu ya hiki nilichokiandaa hapa au kama una wazo lolote kwa kunipata na hii namba

0688665508

Ahsanteni na majukumu mema



Comments