Hizi hapa nyaraka za kisheria za shabiki wa Man United Tanzania aliyebadili jina na kujiita Chicharito


Hizi hapa nyaraka za kisheria za shabiki wa Man United Tanzania aliyebadili jina na kujiita Chicharito

IMG-20150423-WA0014Kitambulisho cha Taifa cha Chicharito

KUNA watu wanapenda mpira hakuna mfano! shabiki mmoja wa Manchester United, aliyekuwa anaitwa Godlisten Anderson Mmari amebadili jina kisheria na sasa anaitwa Godlisten Anderson Chicharito.

IMG-20150423-WA0016

Pasipoti ya kusafiria ya Chicharito

Godlisten ameondoa jina la babu yake (Mmari) na kuweka jina la mchezaji wa Manchester United ambaye kwasasa anacheza kwa mkopo Real Madrid kutoka septemba mwaka 2014, raia wa Mexico, Javier Hernandez maarufu kwa jina la Chicharito.

IMG-20150423-WA0019

Licha ya Godlisten kuwa shabiki wa Manchester United, lakini anampenda mno Chicharito, yaani shabiki wa kutupwa na amefikia hatua ya kwenda mahakamani kujimilikisha jina hilo na kuondoa jina la babu yake mzaa baba! si mchezo aisee!.

IMG-20150423-WA0015IMG-20150423-WA0019 (1)IMG-20150423-WA0017



Comments