Henderson amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.


Henderson amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.

jordan-henderson-liverpool-premier-league_3236347

Na Anwar Binde,

Kiungo wa Liverpool Jordan Henderson amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yiyo wenye thamani ya paundi 100000 kwa wiki.

Tukio nilo limemaliza mazunngumzo ya miezi kadhaa kati ya pande hizo mbili na kiungo huyo wa zamani wa sunderland na utamfanya abakie klabuni hapo hadi 2020.

"Tumekua na mazungumzo ya muda mrefu lakini sasa tumefikia tamati "aliiambia tovuti ya klabu hiyo

"Ni habari njema sana kwangu kusaini mkataba huu na kwa suku za mbeleni kwa klabu hii nadhani miaja michace ijayo tutashinda mataji."alisema.

Matumaini ya Liverpool kushinda taji msimu huu yalizimwa na Aston villa pale walipotolewa kwenye nusu fainali ya kombe la FA.

"tumekuwa vizuri kwa misimu ya hivi karibuni lakini na tumai musa si mrefu unaokuja tutaanza kushindania ubingwa rasmi na makombe mbalimbali "alisema

Liverpool pia walifanikiwa kuwasainisha mshambuliaji Daniel sturridge na kiungo mbrazil Philippe coutinho .Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema,"wamiliki wejizatiti kutengeneza timu ambayo itakua na kuendelea kuwa bora zaidi na kupata ushindi.Tumeona mkataba muhimu ikisainiwa msimu huu na nipo na uhakika chini ya uongozi wa Ayre stewardship tutaona vipaji vingi vikipatikana na kuongezewa katika kikosi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa uingereza alijiunga na Liverpool mwaka 2011 akitokea black cats kwa thamani ya paundi milioni 20.

Kuondoka kwa steven Gerrard mwisho wa msimu kuelekea ligi kuu ya Marekani kuanaacha nafasi kwa Henderson kuwa moja ya ma kepteni watarajiwa klabuni hapo.



Comments