Hazard mchezaji bora wa mwaka England


Hazard mchezaji bora wa mwaka England

Eden Hazard with the PFA Player of the Year trophy              following a ceremony in central London on Sunday

Na Anwar Binde,

Baada ya kusubiri kwa misimu miwili hatimae Eden Hazard wa Chelsea ameibuka mchezaji bora wa mwaka wa England na kutwaa tuzo ya PFA.

Hazard mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 13 na na kusaidia wafungaji (assists) 8 katika michezo 33 ya ligi kuu ya nchi hiyo na kuisaidia timu yake kushika ususkani katika msimamo wa ligi.

Naye Harry Kane mwenye umri wa miaka 21 ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku naye Ji So-Yun wa Chelsea akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake.

Hazard ambaye msimu uliopita aliibuka mshindi kwa upande wa chipukizi alikabidhiwa tuzo yake katika hoteli ya Grosvenor jijini London jana Jumapili. " ninafuraha sana. Nataka siku moja niwe mjichezaji bora kabisa  na nilichofanya msimu huu ni kucheza vizuri na timu yangu imecheza vizuri sana" alisema Hazard baada ya kupokea tuzo hiyo. "sijui kama nastahili kushinda lakini jambo hili ni zuri kwangu. Ni jambo zuri kupigiwa kura na wachezaji kwasababu wanajua kila kitu kuhusu mpira" aliongeza mchezajia huyo.

"Tunaukalibia ubingwa labda hii ndio funguo ya kuelekea ubingwa huo,msimu uliopita tulimaliza nafasi ya tatu lakini kwa sasa ni tofauti ,tunayo nafasi na uwezo wa kuwshinda taji msimu huu"alisema hazard

Hazard alieisaidia timu yake kupata pointi zote 3 dhini ya Manchester united kwa kufunga goli pekee katika mchezo uli[igwa pale Stanford Bridge pia ametajwa katika kikosi cha wachezaji bora 11 wa kulipwa katika ligi kuu ya uingereza huku akiambatana na wachezaji wengine watano kutoka Chelsea ambao ni John Terry,Gary Cahil,Branislav Inanovic, Nemanja Matic na Diego Costa.



Comments