Manchester United na Arsenal zimepata pigo kubwa katika mbio za kunasa saini ya Edinson Cavani katika dirisha la usajili wa kiangazi.
Klabu zote mbili zinaelezwa kudhamiria kumtwaa mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain, ambaye taarifa zinadai hayuko sawa katika klabu hiyo ya Ligue 1.
Lakini siku chache baada ya Cavani kueleza nia yake ya kutaka kubaki Parc des Princes, Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi amesisitiza kuwa staa huyo raia wa Uruguay hauzwi."Ni kijana na mustakabali wa klabu… Anahitaji kujiamini zaidi, lakini mechi yake ya mwisho (ambayo alifunga mara mbili dhidi ya Lille) amedhihirisha kipaji chake. Atakuwa mtu wa Paris msimu ujao," alisema.
Comments
Post a Comment