EDINSON CAVANI KUWASILISHA OMBI LA KUTAKA KUONDOKA PSG …akerwa kuchezeshwa kama winga, Man United yakaa mkao wa kula


EDINSON CAVANI KUWASILISHA OMBI LA KUTAKA KUONDOKA PSG …akerwa kuchezeshwa kama winga, Man United yakaa mkao wa kula

Manchester United imepata matumaini makubwa ya kushinda mbio za uhamisho wa pauni milioni 55 kwa Edinson Cavani baada ya vyanzo vya habari vilivyo karibu na staa huyo kusema atawasilisha hoja ya kutaka kuondoka kiangazi hiki.
Red Devils iko sokoni kusaka mshambuliaji wakati ikijiandaa kuwatema Robin van Persie na Radamel Falcao na bila shaka itafarijika kusikia nia ya Cavani kutaka kuondoka Paris Saint-Germian.
Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Le Parisien la Ufaransa kwamba Cavani hatabaki kwa msimu mwingine PSG kama upangaji kikosi hautabadilika.
"Cavani amekuwa akipangwa kushambulia kutokea upande wa kulia kwa miaka miwili sasa, lakini si nafasi inayomfaa – anataka kuchezeshwa kama mshambuliaji wa kati, nafasi anayopendelea na si hadi asipokuwapo Ibrahimovic," kilisema chanzo hicho.
Kilisema Cavani anataka kuendelea kupangwa kama mshambuliaji wa kati ili kuonyesha ubora wake uliomfanya kuwa kinara wa mabao Italia.
Louis van Gaal ana nia ya kumsainisha mshambuliaji huyo, lakini anakibiliana na ushindani kutoka Arsenal na Liverpool.


Comments