Diego Simione haziwezi Man united,city au Arsenal.



Diego Simione haziwezi Man united,city au Arsenal.

diego 2

Jamie Carragher haamini kama aina ya mpira anaofundisha kocha huyo wa Atletico Madrid kama anaweza kuzivutia klabu kubwa kama Manchester united,city na Arsenal.

Mchambuzi huya ambaye zamani alikipiga klabu ya Liverpool alisisitiza hilo kwa kuwa aina ya soka ambalo timu yake illionyesha wakati wa mechi dhidi ya majirani zao Real Madridi kwamba halikua na mvuto na haliwezi kuzivutia klabu hizo.

"Napenda kumuona akicheza,napenda kuona timu yake ikicheza ni timu ya wanaume kamili inaonekana uwanjani",alisema mchambuzi huyo wa kituo cha sky sports.

diego 5

Haamini kama mpira anaoufundisha unaweza kumfanya akafanya kazi uingeleza bila ya presha.wamepigana sana pale Santiago lakini waliambulia patupu baada ya kubamwizwa goli 1-0 katika ushindi wa jioni kabisa kwa goli safi la Javier Hernandez aliyebadli jina lake moja kwa moja na kuwa Chicharito.

Lakini hakuna timu kama united,city au Arsenal itakayovumilia kwa aina ile ya mpira na kukubali kwamba ule ndo mchezo wanaotaka timu yao icheze.

diego 3

'Kazi aliyoifanya kwa Atletico ni ajabu sana ,rekodi zake ni kubwa sana na zakutisha hata mimi pia namkubali sana lakini hilo halitoshi kumfanya awe na maisha mzuri ndani ya klabu kubwa kama hizi' alisema mchambuzi huyo.

Sidhani kama klabu hizo zitaliangalia hilo ,hata mashabiki walikubali kwamba ule mchezo wa jana ulikua hauna mvuto ule wa wapinzani wa jadi.

 Lakini tuangalie timu unayoyocheza nayo, ina Cristiano Ronaldo ambaye ni mshambuliji htari kwa sasa duniani, Timu lazima icheze ndani zaidi,kujaza watu wengi wakabaji na kuzuia nafasi zote ambazo zinaweza pelekea mipira ya counter attack za hatari na kuweza kusababisha madhara langoni mwako.

Kocha huyo alisema kwamba ameridhishwa sana kiwango walichoonyesha vijana wake jana usiku licha ya kupoteza mchezo huo kwa goli 1-0.

Mchomo wa dakika za mwisho wa Chicharito,ulitenganisha klabu hizo mbili kutoka matokeo ya 0-0 ya mchezo wa kwanza wa robo fainali.

"najiskia furaha sana na timu yangu,vijana wangu wamepigana sana hadi hapo tulipofikia,pia nafurahi kuwa katika timu bora 8 za ulaya ni mafanikio sana kwetu" alisema Diego Simione.

 

 



Comments