DE GEA AENDELEA KUIPASUA KICHWA MANCHESTER UNITED, YAMPANDIA DAU HADI PAUNI 200,000 KWA WIKI …Van Gaal asema kwa sasa ‘boss’ ni De Gea
Manchester United imempa David de Gea ofa ya pauni 200,000 kwa wiki ili kumbakiza kipa huyo Old Trafford.
Kwa ofa hiyo, De Gea atakuwa ndiye kipa anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani na United imefanya hivyo ili kuzima njozi za Real Madrid ambayo imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na usajili wa nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid.
Mkataba wa sasa wa De Gea ndani ya Manchester United unakwIsha kiangazi cha mwaka ujao ambapo Real Madrid inanyatia kumnyakua kwa usajili huru mlinda mlango huyo ili awe mrithi wa Iker Casillas.
"Tumempa ofa nono De Gea," alisema kocha Louis Van Gaal. "Imechukua muda mrefu sasa. "Nataka abaki lakini kwa muda huu mimi sio boss. De Gea ndiye boss, anaweza kusema ndio au hapana. Mnaweza kumuuliza De Gea, sio mimi. Ni wajibu wake kusaini."
United imempa De Gea ofa ya pauni 180,000 kwa wiki pamoja na marupurupu ambayo yatamfanya ampiku kipa wa Manchester City Joe Hart, Gianluigi Buffon wa Juventus, Manuel Neuer wa Bayern Munich na Iker Casillas wa Real Madrid.
Comments
Post a Comment