CHRIS SMALLING AJITIA KITANZI MANCHESTER UNITED


CHRIS SMALLING AJITIA KITANZI MANCHESTER UNITED

Sentahafu wa Manchester United Chris Smalling amesaini mkataba mpya wa miaka minne, klabu hiyo imetangaza.
Nyota huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 25, amejitia kitanzi Old Trafford hadi kiangazi cha mwaka 2019.
Smalling ambaye alisajiliwa kutoka Fulham kwa pauni milioni 10 miaka mitano iliyopita, amekuwa mtu muhimu katika kikosi cha Manchester United chini ya Louis van Gaal.
Van Gaal amesema: Chris ameimarika ndani ya kipindi kifupi tangu nianze kuikochi timu hii na amekuwa 'mwanachama' wa kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Nimefurahi kuwa kuwa amesaini mkataba mpya."


Comments