Chicharito hakamatiki Real Madrid


Chicharito hakamatiki Real Madrid

042615-Soccer-leading-the-line-pi-ssm.vadapt.620.high.0

Na Anwar Binde,

Meneja wa timu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amemsifu mshambuliaji wake Javier Hernandez kwa kuwa katika kiwango bora kabisa na kudai kwa sasa huwezi kumwacha katika kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo ambae anacheza kwa mkopo hapo amefunga magoli sita katika mechi nane na jana usiku alifunga magoli mawili pale Real Madrid ililoichapa Celta Vigo kwa jumla ya magoli 4-2.

Magoli hayo mawili ya chicharito yanamfanya sasa awe na rekodi ya kufunga kila baada ya dakika 83 na ni tofauti ya dakika 2 pekee kati yake na mshambuliaji hatari wa Barcelona lionel Messi ambae anafunga kila baada ya dakika 81.

Chicharito ambae hajui hatma yake itakuaje,kama atasajiliwa moja kwa moja na Real Madrid au atakuwa wapi msimu ujao kwa sababu hayupo katika mipango ya kocha wake wa timu yake inayomliki Manchester united, alisema kwa sasa anaweka umakini mkubwa kwa klabu aliyopo kwa sababu ndiko alikosajiliwa na kuhusu baadae haimuumizi kichwa kwa sasa bali anajalibu kuzitumia vizuri dakika chache anazopewa uwanjani

Ushindi wa jana umepunguza pengo na kufikia pointi 2 kati ya Barcelona na Real Madrid na zikiwa zimesalia mechi 5 ligi kumalizika.



Comments